Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Morogoro Afande Sele amesema leo
tafsiri ya msemo wake ‘wasafi wataonekana wachafu’ ambayo aliitoa siku
za karibuni baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda
kutangaza awamu ya kwanza ya majina ya watu ambao wanatuhumiwa
kujihusisha na matumizi ya Madawa ya kulevya.
Kauli hiyo ilitafsiriwa vibaya na mashabiki wa Diamond wengi wakidhani
mkongwe huyo naye naamini kwamba WCB wapo kwenye sakata hilo.
Kupitia list mpya ya RC Makonda ambayo ameitoa leo na kutaja majina ya
watu wakubwa akiwemo Yusuph Manji, Mchugaji Mwajima, Iddi Azzan na
wengine, Afande Sele ameweka bayana nini alikuwa anakimaanisha kwenye
kauli yake hiyo.
“Juzi kati niliposema kuwa kwenye hili sakata la MAPAPA na MAPUNDA
wa’Unga’kama kweli braza Paul yupo’serious’….basi hata wale WASAFI
wataonekana WACHAFU….wenye akili zao timamu walinielewa vyema….lkn
vibichwa panzi walitafsiri kiudaku na kichonganishi tu wakimaanisha neno
wasafi na wale wasafi wao wa mbagala…nadhani sasa tumeanza
kuelewana…..NAONA MBALI KWA DARUBINI KALI…..wacha ‘parry’iendelee,”
aliandika rapper huyo Instagram.
0 comments:
Post a Comment