Belle 9 Afunguka Umaskini Ulivyomfanya Apokonywe Mpenzi Wake

Wimbo, Sumu ya Penzi uliomtoa Belle 9, ulikuwa ni true story ambayo hatoweza kuisahau kamwe.
Aliuandika baada ya mpenzi wake kummwaga na kuanzisha uhusiano na mtu aliyekuwa akimfahamu.
“Ilinichukua muda sana kuzoea ile hali,” Belle 9 alisema kwenye mahojiano na Lil Ommy kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM.
“Kwasababu kitu ambacho kilichokuwa kinaniuma ilikuwa katoka kwangu halafu kaenda kwa mtu ambaye namfahamu kabisa, na yule mtu maisha ya kwao na maisha ya nyumbani ni tofauti. Yule alikuwa hata siku tukienda kwenye mpira kila siku anabadilisha six, anabadilisha jezi, sisi ndio tulikuwa wale watu ambao tunarudia hizo hizo kila siku,” aliongeza.

0 comments:

Post a Comment