Taarifa za Mchekesha Kansime Kukamatwa na Madawa ya Kulevya London..Ukweli Huu Hapa

Kuna picha inasambaa kwenye mitandao kuanzia ikionyesha sehemu ya habari iliyoandikwa na mtandao uitwao METRO na inasema Mwigizaji/Mchekeshaji wa Uganda Anne Kansiime amekamatwa na Polisi kwenye uwanja wa ndege London akiwa na dawa za kulevya kilo mbili.

Ni habari zilizowashtua wengi lakini ukweli tumeupata, Anne hajakamatwa na yeye ni mzima wa Afya nyumbani kwao Kampala Uganda na usiku wa leo anatarajia kufanya show inayohusiana na sanaa yake.


Baadhi ya mitandao imekanusha na kusema kuwa sio kweli lakini pia baada ya hili nikapita kwenye ukurasa wa Instagram wa Anne kansime na kwenye picha ya mwisho kupost alicomment kusema yuko salama baada ya mwimbaji Irene Namubiru kumuuliza.


Kupitia ukurasa wake wa Twitter @Kansiime256 Anne aliandika pia kwamba kuwa yuko uwanja wa taifa Uganda tayari kwa show yake usiku wa leo.

Kamanda Sirro: Tulipata Taarifa Huenda Masogange ni Kati ya Wauzaji au Wasafirishaji wa Unga (Video)

 
Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amedai kuwa sababu ya kumshika mrembo maarufu wa video za muziki nchini, Agnes ‘Masogange’ Gerald ni kupata taarifa kuwa huenda akawa mmoja wa wauzaji, watumiaji ama wasafirishaji wa dawa za kulevya.

“Kwahiyo tumemhoji, tumemsachi na tumempeleka kwa mkemia wa serikali,” Sirro amewaambia waandishi wa habari Alhamis hii.

“Kwahiyo tunasubiri tupate majibu ili tuweze kuchukua hatua. Hatua yenye inaweza kuwa ni kumpeleka mahakamani kwa kosa lake ambalo litakuwa limebainika.. tumeona amekuwa na tabia ambazo sio nzuri au itakavyokuwa vinginevyo kutokana na hatua ambayo kutokana na ushahidi tutakaokuwa tumeupata,” ameongeza.

Masogange alikamatwa February 14, 2017 na kufanya idadi ya watu waliokamatwa hadi sasa kufikia 349.

Fahamu Mambo Yanayowachizisha Wanawake...!

HAKUNA aliyeaibika wakati akijaribu kufanya jambo kwa faida yake. Siku zote kufanya jaribio ni mwanzo wa kuelekea kwenye ufanisi mzuri wa jambo husika.
Rafiki zangu, ni vema nawe ukajiwekea utaratibu wa kujaribu kufanya mambo ambayo unadhani huyawezi, lakini yakileta matokeo chanya yatakuwa na faida kubwa kwako.
Kujaribu kupo katika mambo mengine mengi ya kawaida – ya kibinadamu. Katika mambo mbalimbali ya kila siku. Ukianza na kupata matokeo mazuri, unakuwa mshindi na bila shaka unakuwa umefanikiwa.
Hali ni tofauti katika suala la mapenzi, huku hakuna kujaribu – ni kuamua tu! Hata hivyo, wakati unaamua mambo yako yanayohusu mapenzi ni lazima kichwani mwako utambue kuwa unafanya kitu kwa ajili yako na mtu mwingine (mpenzi wako).
Hapo ndipo kazi inapokuja. Kwa maneno mengine, wakati ukijifikiria wewe katika ulimwengu wa mapenzi, unatakiwa pia kumfikiria mpenzi wako.
Kwa bahati mbaya, katika eneo hili, wanaume wengi huwa hawafikirii sana namna ya kuwafurahisha wenzi wao. Wanahisi ni suala linalowahusu wanawake pekee. Ni kosa.
Kama mwanaume lazima upate wakati wa kujua unatakiwa kufanya nini kwa ajili ya kulifanya penzi lako lizidi kuchanua.
Hapa katika Love Moment, nimekuandalia mambo ambayo wanawake wengi wanavutiwa zaidi kutoka kwa wanaume.
Je, wewe ukoje? Una sifa hizo? Hebu twende pamoja katika mada hii ambayo bila shaka itakutoa matongotongo.

USAFI BINAFSI
Asilimia kubwa ya wanawake wanapenda sana usafi. Ni aghalabu sana kukutana na mwanamke asiyejipenda. Ndiyo maana wanaitwa mapambo ya nyumba au ua la nyumba! Ni kwa sababu ya hulka yao ya kupenda sana usafi.
Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini kuwa na wewe. Hata nyumbani kwako, lazima uishi katika nyumba safi. Hata anapokuja kukutembelea, anakuta mazingira masafi kuanzia sebuleni hadi chumbani.
Anapokukuta katika hali ya usafi, inakuwa rahisi zaidi yeye kuanzia hapo alipokukuta na kuendelea mbele.
KUJIAMINI
Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na mwanaume ambaye anajiamini – mwenye uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza sawia. Siyo anayebabaika.
Suala la msimamo binafsi, kwa mwanamke ni kubwa kuliko hata kumnunulia manukato mapya. Mathalani unakuwa naye katika mtoko, angependa kukuona ukiwa katika hali halisi ya maisha yako, usiyeyumbishwa na mwenye kutoa maamuzi yasiyoyumba.
Wakati mwingine, mwanamke anaweza kukupima hata katika jambo ambalo amekosea yeye, ataangalia unavyotoa maamuzi yako, lakini pia atafuatilia kuona kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha.
Anataka kuona msimamo wako muda wote. Mwenye kujiamini na mawazo yasiyo na matege wala makengeza!

KUJITETEA
Kipengele hiki hakina tofauti kubwa sana na kilichopita, lakini hapa ni kwenye upande wa kujitetea zaidi. Wakati unapodai haki yako mbele ya mwanamke wako, suala la kujitetea linapewa nafasi kubwa sana.
Wanawake hawapendi kuwa na wanaume ambao wapo tayari kuonewa. Wanataka wenye uwezo wa kusimama kidete kuona haki zao hazichukuliwi kirahisi.
Hili si suala la kutetea tu haki yako pekee kama mwanaume, bali inapobidi kusimamia haki ya mwanamke wako. Nisieleweke vibaya katika hili, lakini mwanaume imara ni yule ambaye ana nguvu – anafanya mazoezi na ambaye yupo tayari kwa lolote!
Inapowezekana, uwe na uwezo wa ‘kuzichapa’ ikiwa mtakutana na vibaka au watu wabaya wenye lengo wa kukudhuru/kuwadhuru au kumdhuru mpenzi wako.
Mwanaume aliye ‘fiti’ ni chaguo la wanawake wengi. Si mnyonge. Mpole kupitiliza na aliye tayari kuonewa! Huyu hana nafasi.
KUJALI
Wanawake wanapenda sana wanaume wanaojali. Wanawaona wao ni kila kitu na wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa ya kumkwaza mpenzi wako. Mjali mpenzi wako kwa kila hali.
Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa sana ya kuendelea kudumu katika uhusiano hai.

UKARIBU
Kati ya vitu vinavyowapa mshawasha mkubwa wanawake ni pamoja na kusogezwa karibu. Hapa ni kuwa naye katika mambo mengi unayoyafanya kila siku.
Ni vizuri kuwasiliana naye mchana, ukitaka kujua aina ya chakula alichokula siku hiyo au ikiwezekana mchagulie. Ni mambo madogo sana lakini yanayoongeza nakshi katika mapenzi.
Yapo mengi sana ambayo kwa kuyafanya utakuwa umemsogeza mpenzi wako karibu yako. Hebu tumia ubunifu wako ili uweze kuteka hisia za mwenzi wako kisawasawa.

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya: Watoto Hawa Wawasikitisha Wengi (Video)

Moja kati ya jambo lililowasikitisha wengi Jumatatu hii katika mkutano ulioandaliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ni pale walipotajwa watoto wawili wa kike ambapo mmoja ana umri wa miaka 14 na mwingine 16 kuwa walikuwa wakitumia dawa za kulevya kwa takriban miaka mitano.

Wakati huo huo mtoto mmoja mwenye miaka 16 aliongeza kuwa mbali na kutumia madawa hayo lakini pia yamempelekea kuambukizwa virusi vya ukimwi kwa kuwa wakati mwingine ilimlazimu kujiuza ili apate fedha za kununulia dawa hizo.

Wakati huo huo Kamishna mpya wa kupambana na Madawa ya kulevya, Rogers Sianga ameahidi kuwasaidia watoto hao kwa kuwapatia huduma bora za afya ambazo zitawasaidia wasirudi tena kwenye janga hilo.

Orodha hiyo ya tatu iliyotolewa leo na Mh. Makonda ina idadi ya majina 97 ambapo kati yao amedai kuna majina ambayo yatawasha moto zaidi huku akiahidi kuwa kuna awamu nyingine nne zimebakia za kutoa majina hayo.

OnAIR: Ataemchukulia Irene Uwoya Mwanaume, Wanaume wanaokwenda Saluni je? (VIDEO)

Mtangazaji Millard Ayo alikaa kwenye studio yake na kumuhoji Mwigizaji wa Tanzania Irene Uwoya aliekubali kuelezea ishu zake mbalimbali kuhusu maisha.
Atafanyaje pale Mwanamke mwingine atapomchukuliwa Mwanaume wake? Wanaume watano wenye sura “mbaya” wanaomvutia? kasemaje kuhusu Wanaume wanaokwenda Saluni? Ukimtaka unatakiwa kufanyaje? hayo ni baadhi tu ya maswali aliyoyajibu Irene… mtazame kwenye hii video hapa chini

Vigogo Watema ‘Moto’ Dawa za Kulevya...!!!

Siku mbili baada ya kuwa madarakani, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga amesema hakuna mtu atakayepona baada ya kubainika akitakatisha fedha zilizopatikana kwa njia ya dawa za kulevya.
Sianga amesema hayo katika mkutano ulioitishwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambapo pia alikabidhiwa na Makonda majina 97 ya watu wanaojihusisha na dawa hizo.
Kamishna huyo amesema atakayefanya biashara ya dawa za kulevya au utakatishaji wa fedha atachukuliwa hatua kwa sababu sheria mpya ya udhibiti inawapa uwezo wa kukamata hadi mali ambazo atakayepatikana na hatia amezichuma.
Kamishna wa Intelijensia wa mamlaka hiyo, Frederick Kibuta amesema katika kutekeleza majukumu ya taasisi hiyo, watazingatia sheria katika kila hatua.
Amewataka wananchi kufahamu sheria kwa sababu kutokujua hakutoi nafasi ya kuzivunja.
“Popote walipo tutawafikia na tutawachukulia hatua, hakuna atakayebaki salama katika hili,” amesema Kibuta.
Awali, akizungumza katika mkutano huo, Makonda amemuomba Spika wa Bunge, Job Ndugai aweke kipimo maalumu kitakachokuwa kinawapima wabunge kabla hawajaingia bungeni ili wabainike kama wanatumia dawa za kulevya au la.
“Kaka yangu Ndugai alisema ana nia ya kuweka kifaa maalumu kuwapima wabunge kama wanatumia dawa za kulevya au la, hivyo atimize nia yake hiyo ili kama na huko wapo tuwanyofoe,” amesisitiza Makonda.

FULL VIDEO: Awamu ya 3 ya Paul Makonda sakata la dawa za kulevya

Leo February 13 2017 mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amezungumza kuhusu vita ya dawa za kulevya awamu ya tatu, awamu hii Paul Makonda amekabidhi majina 97 ya wanaotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya kwa kamishna mkuu wa mamlaka ya kupambana na kuzuia dawa za kulevya, William Sianga. Unaweza kutazama kila kitu kwenye video hii hapa chini

U HEARD: Irene Uwoya afafanua ishu ya kupenda wenye sura mbaya

Baada ya mwigizaji Irene Uwoya kusema kuwa anapendelea zaidi kuwa na wanaume wenye sura mbaya, leo kupitia XXL ya clouds FM, Soudy Brown amepiga naye stori na ameifafanua zaidi kauli kauli.
Nawapenda wanaume wenye sura mbaya kwa sababu wanajua mapenzi na wanaogopa kuachwa, mtu mwenye muonekano mzuri yuko busy na kujitengeneza lakini mbaya yeye mkiwa sehemu akili inakuwa pale’;-Iren Uwoya
Bonyeza play hapa chini kusikiliza Full Stori

Lissu Awaonyesha Polisi Kuwa Yeye Ni Zaidi ya Kiburi,Adai Maneno ya Uchochezi Katamka Kweli na Hajafanya Kosa..!!!

Baada ya kukaa mahabusu kwa siku nne, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema kuwa maneno anayoshtakiwa kwa kuyatamka ni ya kweli na kuwa siyo kosa.
Lissu ambaye yupo nje kwa dhamana, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka manne ya kutoa maneno ya uchochezi na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa.
Awali, kabla ya kupandishwa kizimbani mbunge huyo aligoma kula akiwa mahabusu ya polisi kwa mujibu wa wakili wake, Peter Kibatala.
Kutoka kwa Lissu kulifuatia kasoro za kuandaa kiapo kuwa mojawapo wa sababu zilizoifanya Mahakama hiyo kutupa pingamizi la dhamana lililowekwa na upande wa Serikali.
Mbunge huyo amepandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka manne ya kutoa kauli za uchochezi, ambapo upande wa mashtaka uliwasilisha ombi la zuio la dhamana lililoambatana na kiapo cha Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Wilaya Ilala, Mrakabu Msaidizi (ASP), Denis Mjumba.
Hata hivyo, mahakama hiyo imetupa pingamizi la dhamana pamoja na mambo mengine kutokana na kasoro katika kiapo hicho.
Akitoa uamuzi wa pingamizi hilo, Hakimu Mkazi, Huruma Shaidi ameainisha mambo matatu yaliyomfanya kulikataa pingamizi hilo na kuamua kumwachia kwa dhamana mtuhumiwa.
Lissu ametimiza masharti hayo na kudhaminiwa na Diwani wa Kata ya Tabata wa chama hicho, Patrick Asenga hivyo akaachiwa huru.

FULL VIDEO: Kabla na baada ya Wema Sepetu kuachiwa kwa dhamana

Leo kwenye Mahakama ya hakimu mkazi kisutu Dar es salaam alifikishwa Mwigizaji Wema Sepetu ambaye kuanzia wiki iliyopita alikua akishikiliwa na jeshi la Polisi kwenye sakata la dawa za kulevya.
Mahakamani Kisutu leo imekubali kutoa dhamana ya mwigizaji huyo ambapo imehusu Wadhamini wawili na milioni 5 ambapo pia tarehe 22 mwezi huu anarudi tena Mahakamani kusikiliza majibu ya Mkemia Mkuu wa Serikali kujua kama ni mtumiaji wa dawa za kulevya, video ya ilivyokua Mahakamani itazame kwa kubonyeza play hapa chini

Viongozi wa Dini Wamuunga Mkono Makonda...!!

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema dawa za kulevya zinateketeza nguvukazi ya Taifa, jambo ambalo halipaswi kuachwa liendelee kumea.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Sheikh Alhad amesema baraza la viongozi wa dini la kupambana na dawa za kulevya nchini linaunga mkono juhudi zifanywazo na Serikali kupambana na jambo hilo.
“Suala la matumizi ya dawa za kulevya limekuwa kikwazo cha maendeleo nchini kutokana na nguvu kubwa ya Taifa ambayo ni vijana kujihusisha na utumiaji wa dawa hizo,” amesema.
Amesema kuwa wanawataka viongozi wengine wa umma kuiga mfano wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wa kupambana na uovu wa uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya ambao ni janga kwa Taifa.
“Tunawaomba wananchi wote kuunga mkono suala hili pamoja na kuonyesha ushirikiano wa kutosha kwa wale walioamua kujitoa kwa ajili ya nchi yetu.”
Katibu wa baraza la viongozi wa dini la kupambana na dawa za kulevya nchini, Padri John Solomoni ameitaka Serikali kushughulikia suala hilo kwa umakini ili lisiibue manung’uniko miongoni mwa wananchi ambao hawana hatia.
Padri huyo amewataka viongozi wanaochunguza suala hilo kuwa makini ili wasiharibu haki ya mtuhumiwa.
“Ikumbukwe kwamba wanaotajwa ni watuhumiwa, huenda baada ya uchunguzi wakabainika kuwa hawakuhusika. Baada ya kugundulika kuwa hawana hatia na itakuwa vigumu kurudisha waliyokuwa nayo hapo mwanzoni,” amesema.
Kwa takriban wiki moja sasa, watu mbalimbali wamehojiwa na polisi kuhusiana na ama utumiaji wa dawa hizo au uuzaji katika vita inayoendeshwa na mkuu wa mkoa huo.