MUUZA sura kwenye video za Bongo Fleva ambaye pia ni mtangazaji wa Kituo
cha Redio cha Choice FM, Gift Stanfod ‘Gigy Money’ hivi karibuni
amefunguka kuwa, katika maisha yake, ipo siku ataachana na mambo yote
yasiyompendaza Mungu kisha kumtumikia muumba wake.
Akipiga stori mbili tatu na Global Publishers, Gigy aliweka wazi kuwa,
katika maisha ya mwanadamu, hasa kijana hukumbana na changamoto nyingi
za kimaisha ambazo wakati mwingine humfanya kumkosea muumba wake, lakini
inafikia hatua anaamua kuacha kila kitu na kufanya yanayompendeza
Mungu.
“Unajua sometimes tunadondoka dhambini, lakini si kwa mapenzi yetu,
binafsi ipo siku tu, nitaachana na mambo ya kidunia na kusimama kwa
Mungu,” alisema Gigy asiyeishiwa vibwanga.
0 comments:
Post a Comment