Sasa leo February 01 2017 imetolewa taarifa kupitia kwa mkurugenzi wa Idara ya habari maelezo Dr. Hassan Abbasi ikiwa ni baada ya kuipata barua ya Mwanahalisi kuomba radhi, taarifa ya leo imeainisha hatua mbili zilizotangazwa dhidi ya gazeti hilo.
- Wachapishaji na wahariri wa gazeti la Mwanahalisi wanapewa onyo kali na hatua kali zaidi zitachukuliwa iwapo wateendeleza uandishi unaokiuka maadili ya kitaaluma na sheria za za nchi.
- Kwa kuwa habari husika ilichapishwa kwenye ukurasa wa mbele katika toleo lililopita, Mhariri anaagizwa bila kukosa, achapishe barua ileile ya kuomba radhi katika ukurasa wa mbele katika tolea lijalo la February 6 2017 la gazeti la Mwanahalisi.
0 comments:
Post a Comment