Msanii wa muziki Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewaduwaza
ndugu, jamaa na marafiki waliofika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere kumpokea baada ya kutua kutokea Sauzi akiwa peke yake,
tofauti na ilivyotarajiwa kuwa angerejea na mzazi mwenzake, Zarina
Hassan ‘Zari’.
Awali zilivuja taarifa kuwa, Diamond amekwenda Sauzi kumchukua Zari na
mtoto wao aliyezaliwa hivi karibuni, Nillan ili waje kufanya sherehe
kidogo.
Kufuatia taarifa hizo, Jumatatu iliyopita, nyakati za jioni, watu wa
karibu na Diamond walifika ‘airport’ kuwapokea lakini kilichowashangaza
wengi ni kumuona anatoka mwenyewe na mabegi yake, jambo lililowafanya
wahisi kuna kitu.
“Hee, mbona yuko peke yake sasa? Zari na watoto wako wapi sasa? Au
wamezinguana?” alisikika akisema mmoja wa akinadada waliokuwa uwanjani
hapo.
Mbali na dada huyo, wengi walionekana kunong’ona kuonesha kutoamini
wanachokiona na kwa kuwa Diamond alijua kuwa kawaangusha kwa kutokuja na
Zari, hakuwa na mbwembwe zaidi ya kwenda kwenye gari lililokuwa
limeletwa na kijana aitwaye Q Boy, wakaondoka zao.
0 comments:
Post a Comment