Kudadeki..Obama Amuibukia Trump,Amshambulia Kwa Kauli Hizi Juu ya Agizo Lake la Kuwazuia Waislamu Wasiingie Marekani

RAIS mstaafu Barack Obama ameibuka na kuzungumzia siasa ikiwa ni mara ya kwanza tangu astaafu urais – akiunga mkono maandamano yanayosambaa nchini kote kupinga agizo la Rais Donald Trump kuhusu uhamiaji.
“Rais Obama amesikitishwa na kiwango cha matukio yanayotokea hivi sasa kwenye jamii mbalimbali nchini,” kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi yake ya rais mstaafu.
“Wananchi kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kukusanyika, kuandaa na kufanya sauti zao zisikike na maofisa waliochaguliwa, ndicho hasa tunachotarajia kukiona pale maadili ya Marekani yanapokuwa matatizoni,” alisema Obama.
Hata hivyo, Rais huyo mstaafu hakuingia ndani zaidi kuhusu matamko ya Trump – yakiwamo ya kuzuia ruhusa ya wakimbizi kuingia nchini na kusimamisha uhamiaji wa watu kutoka nchi saba duniani zikiwamo Iraq na Syria.
Badala yake, Obama ambaye ana haki ya kuingilia kati pale mambo ya kisiasa na hasa ‘masuala nyeti’ yanapokuwa hatarini, aliomba “kulinganishwa kwa uamuzi wa sera zake za nje na za Trump.”
“Kwa kuzingatia mlinganisho na uamuzi wa sera za nje za Rais Obama, kama tulivyosikia kabla, kimsingi rais hakubaliani na suala la ubaguzi dhidi ya watu kwa sababu ya imani yao au dini,” kwa mujibu wa taarifa.
Katika mkutano wake wa mwisho na waandishi wa habari, Obama alisema anaweza kuingilia “nyakati fulani wakati anapokuwa anadhani kwamba maadili yetu ya msingi yamo hatarini.
Obama kwa kiasi kikubwa alishambulia moja kwa moja kauli ya Rais Trump: kwamba “Sera yangu ni sawa na alichokifanya Rais Obama mwaka 2011 alipopiga marufuku viza kwa wakimbizi kutoka Iraq kwa miezi sita.”
Gazeti la Washington Post lilielezea kauli hiyo kama madai yasiyo na kichwa wala miguu, “kwa sababu utawala wa Obama haukupata kuzuia Wairaqi kuingia nchini. Utawala huo ulibana uingiaji wa Wairaqi nchini mwaka 2011 wakati ilitangaza majina yaliyokuwa kwenye kanzidata ya nchi, baada ya Mwiraqi ambaye alikuiwa na hifadhi nchini, kubainika kuwa alipata kutega mabomu barabarani nchini mwake”.
Hata hivyo, msaidizi wa Obama hakujibu swali la alikokuwa Rais huyo mstaafu wakati akitoa taarifa yake hiyo.

0 comments:

Post a Comment