Roma Atolewa Bonge La Povu na Mkewe Mama 'Ivan' Kisa Hela ya Madee

Rapper Roma Mkatoliki ameonekana kukerwa na mkewe mama Ivan.

Mkewe huyo ambaye kwenye mtandao wa Instagram anatumia jina la @mrs_roma2030 amepost kwenye mtandao huo kipande cha video akiimba wimbo wa ‘Hela’ wa Madee na kuandika,
“Mengi nimepitia nikiwaadisia wengine mtalia sana/inamengi dunia usipoangali watawakatisha tamaa..heeee/laaa @madeeali.

Kitendo hicho kimeonekana kumuumiza Roma ambaye aliamua kutoa dukuduku lake kwa kuandika comment iliyowashangaza mashabiki,
“Shobo hilo mxiuuuuuu kwa wimbo gani basi nawe ukaenda kujiiimbiiishaaaa!!!??? MXIUUU wajitia kuuvalia na Ushungi mwana mkosa kazi wewe!! Kwa msanii gani basi….Msanii Maandazi huyo. Nyote namiona washamba tu. Mxiuuuuuu.”

0 comments:

Post a Comment