Nakumbuka miaka ya zamani lulu nae alikua hivi hivi hashikiki, kila club
yeye, kila rafiki yeye, mtoto alikua hashikiki mpaka mama yake akainua
mikono, lulu anatoroka kwao usiku wa manane anaenda kwa wanaume, maisha
yake yalikua kwa mashosti, shule akaikacha, umaarufu ukampa kichwa
akajiona yeye ndio yeye, siku ya siku ikatokea ajali ( wote mnajua
yaliyotokea) akawekwa rumande miezi kadhaa, Lulu akawa lulu machozi,
alikonda ,maisha yake kila siku vilio, mashost wote wakamkacha, hakuna
aliyekua na habari nae alipokua rumande, kila mtu alimkashifu kwa style
yake, lulu akawa lulu machozi, rafiki yake akawa BIBLIA na rosali, lulu
akamgeukia Mungu, Mungu si athumani akasikia kilio chake akatoka kwa
dhamana, akawa HURU, tokea hapo hatukuwahi kumsikia lulu na marafiki wa
ajabu ajabu, lulu club akawa haonekani,familia yake ndo ikawa rafiki
yake pamoja na muna love na baadhi ya mastaa wachache, sasa hivi huwezi
kukuta picha za lulu akilewa hovyo kama zamani (kuna tetesi aliacha
pombe) , lulu akabadilika kabisa akawa mpya, sasa hivi katulia na
boyfriend wake.
Back to wema, nadhani ni wakati wa mashabiki wa wema waache kushabikia
upuuzi, hivi karibuni wema amekua na scandal chafu za kubadili wanaume
na kuongozana na mashoga wasio na focus na maisha, wema kampani yake
wanaume mashoga, mashangingi na wauza madawa (pengine hii imemcost)
inawezekana mdada wa watu hata hausiki ila kwa kuwa anaongozana na wezi
na yeye lazima wamuhisi mwizi, nadhani hili litakua ni funzo kwake, mama
yake kashalia sana na wema mpaka wamegombana ila wema hasikii,anaishi
maisha anayotaka yeye, pengine ni hao hao marafiki zake wa karibu
wamemchomea, MIMI NADHANI WEMA AKIWEKWA NDANI KAMA MIAKA MIWILI AU
MITATU nadhani atabadilika, najua watu watafikiria vibaya ila SIO KILA
JAMBO BAYA LINATOKEA KWENYE MAISHA YETU KWA NIA MBAYA,mengine yanatokea
kama funzo au baraka, mi nadhani ni wakati wa wema kukubali matokeo na
kukaa ndani, im telling you akitoka wema atakua anaimba GOSPEL, huruma
zenu zitamponza, jela hapaui ni sehemu ya kujifunza.
0 comments:
Post a Comment