Shoga Chakula Hakiliwi Gizani....!!!!

EEE heiiyaaa…shoga yangu ni Jumanne nyingine tamu hadi kumoyo, tumekutana tena. Najua wengi mtakuwa na furaha kwa kuwa leo ndo’ tunaukata mwezi wa kwanza na kesho tunaanza mwingine, si ndiyo!
Basi kiafya shoga yangu ni kama ulivyoniacha wiki jana na najua na wewe ni mzima ila kama mgonjwa ni jambo la kuombeana tu! Shoga si unakumbuka wiki iliyopita niliongea na wale wenzangu na mimi ambao kitu kidogo wanachoshwa na chakula cha usiku? Manung’uniko mengi utadhani analazimishwa kuchomwa sindano, inahuu?
Basi shoga yangu baada ya kuandika tabia za wanaume na wanawake kukataa kula chakula cha usiku kwa kisingizio cha kuchoka, nilipata meseji nyingi, tena wengine wakaniambia wamewaonesha waume/wake zao na wamejirekebisha.
Kuna watu walikuwa na shida jamani hee! Tena kuna wengine walikuwa wameshaanza tabia ya kuchepuka, kisa uvivu wa waume zao, aibu! Shoga sasa wiki hii nimepata meseji kutoka kwa msomaji wangu mmoja anayefahamika kwa jina la Hanifa kutoka Tanga.
Ameniambia anafurahishwa sana na mada zangu na zimekuwa zikimfunza sana. Kikubwa alichotaka niongee na wewe pia ukisome na ufanyie kazi ni hizi tabia za wanaume kupenda kula chakula gizani. Meseji yake ilikuwa inasema hivi; shoga mimi ni mama wa mtoto mmoja lakini tangu nimekuwa na mume wangu sasa yapata miaka mitatu.
Zamani mume wangu alikuwa akipenda sana kula chakula cha usiku na mimi kwenye mwanga lakini hivi ninavyokuambia ana zaidi ya mwaka kila tukila naye chakula cha usiku anataka gizani. Naomba nishauri kwani nikila chakula gizani wala sishibi zaidi ya kushinda na njaa nifanyaje shangazi yangu?
Kwanza nikupe pole yako maana hawa wanaume wetu lol! Hivi jamani mkikimbiwa mtu akaenda kula chakula kwenye mwanga na mtu mwingine mtasema nini? Hamjui raha ya chakula au? Mbona zamani tangu umuoe mlikuwa mkila chakula kwenye mwanga?
RAHA YA CHAKULA
Shoga kwanza nikung’ate sikio kwa wewe ambaye unakaa tu hujui raha ya chakula. Ukiona wengi wapo kwenye ndoa zao na wanapenda kula chakula gizani, ujue wanawatoto lakini ukiona mtu hana watoto au watoto wana chumba chao, yeye kwenye kula chakula cha usiku anataka kula gizani, ujiulize huyo mwenzako vipi?
Shoga raha ya chakula ukile kwenye mwanga peupee peee! Kama kuna minofu uione na uitafune utaona raha yake. Kula chakula gizani ni sawa na kwenda uwanjani kucheza mpira wakati mpira wenyewe umeusahau nyumbani au kwenda bafuni kuoga unavua nguo zote sabuni umeisahau ndani, inahu?
HESHIMU CHAKULA
Chakula shoga yangu kina heshima yake, kama unaheshimu vitu vingine na ndiyo maana ukila chakula kwa wakati wake, matokeo yake yanatokea unaitwa baba ati, upo? Jenga mazoea na tenga muda wa kupeana chakula tena kwa kukiheshimu na kukipangia ratiba kama unavyopanga ukiwa ofisini kwako, umenipata shoga?
HAMA MAZINGIRA
Shoga chakula si lazima kiliwe kwenye meza hiyohiyo kila siku au mna zaidi ya mwaka mnakula chakula kwenye meza hiyohiyo utadhani hamna ‘fenicha’ nyingine mjini loool! Shoga jenga tabia ya kutoka na mwenzako kwenye hoteli au sehemu nzuri ambayo mnaweza kupata chakula chenu cha usiku hata kama hamtalala huko basi kubadilisha mazingira ya meza. Raha ya mbuzi au kuku siyo kumla kwa mkono wa kushoto au kulia bali mikono yote, upo?
SAFISHA UWANJA
Huwezi jua shoga, wengine wanaamua kula chakula gizani kwa kuogopa uwanja. Utakuta mwanamke mwenzangu msafi, akivaa anavyonukia utadhani amezaliwa na pafyumu ila mkalishe kwenye chakula cha usiku, we we weeee!
Utakimbia mbona! Shoga jenga mazingira ya kusafisha uwanja wako kila baada ya siku kadhaa. Uchafu hasa kwa sisi wanawake haufai shoga yangu. Tena ukute siku nzima upo kwenye mihangaiko, ukirudi hata ujisugue na sabuni iliyochanganywa na pafyumu na magadi kutoka wapi shoga lazima utanuka tu. Kwa nini usikimbiwe?
Raha ya chakula, mumeo akikute kwenye sahani ambayo ni safi, haina uchafu wa aina yoyote tena ale peupe bila giza, umenipata? Shoga najua nimeongea mengi sana ila kwa leo nahisi kiu imenibana na naomba niishie hapa, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri zaidi ya hapa, upo?

0 comments:

Post a Comment