Mtangazaji wa kipindi cha Lavidavi cha Choice FM, Gigy Money amekanusha
uvumi ambao ulizagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa anataka kuokoka.
Taaifa hizo zilidai kuwa video queen huyo anataka kuokoka ili kufuta mabaya aliyoyafanya katika kipindi cha nyuma.
Akiongea katika kipindi cha Star News cha Star TV wiki hii, mrembo huyo
amedai hana mpango huo huku adai labda abadili dini kumfuata mpenzi wake
wa sasa Mo J.
“Kusema kweli Gigy kama Gigy Gigy hana mpango wa kuokoka, niokoke
kwanini labda nibadili dini kwa sababu ya mpenzi wangu wa sasa lakini
sio kuokoka,” alisema Gigy.
Pia video queen huyo amedai kwa sasa anapata deal za matangazo mengi ya nguo kutokana mwonekano wake wa mwili.
0 comments:
Post a Comment