Afande Sele amefunguka na kusema kama jambo hili litafanywa kwa haki na umakini basi huenda hata wale wasafi wakaonekana ni wachafu.
Afande Sele ameonyesha wasiwasi juu ya sakata hili la madawa ya kulevya ila amesisitiza kuwa kama kweli litafanyikwa kazi kwa umakini mkubwa basi kuna kundi kubwa la watu ambao wanaonekana ni wasafi kuchafuka kutokana na sakata hili.
"Katika hili sakata la MAPAPA na MAPUNDA ya unga kama kweli braza Paul yupo 'serious' na sio 'Matango Pori'kama tulivyoona katika masakata mengine, huenda hata wale WASAFI wakaonekana wachafu...kila la kheri Mr Paul....RiP dada Amina...wacha party ianzeee" aliandika Afande SeleKauli hii ya Afande Sele imekuwa ni kauli tata na imeibuka mjadala kwa baadhi ya mashabiki katika kuitafsiri wengine wakisema Afande Sele amezungumzia wasanii ambao wapo chini ya label ya WCB Wasafi chini ya Diamond Platnumz huku wengine wakisema amezungumzia watu ambao wanaonekana ni wema katika jamiii kumbe si wema bali ni wachafu kwa matendo yao kwa kujihusisha na biashara za dawa za kulevya.
0 comments:
Post a Comment