Linah Sanga afunguka nakumtaja anaye mnyima usingizi

Linah Sanga
Msanii Linah Sanga amefunguka na kuwataja wasanii ambao wanamyima usingizi na kusema hao ndiyo washindani wake kwenye muziki wa bongo fleva kwa sasa.
Linah Sanga alisema hayo kupitia kipindi cha ‘Ngaz kwa Ngaz’ na kudai kuwa licha ya muziki wa bongo fleva kuwa na idadi kubwa ya wasanii wa kike sasa tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma haimuumizi ila anapata changamoto ambazo zinamfanya aumize kichwa na kukosa usingizi kutafuta kitu kipya cha kipekee.
“Kwa sasa hivi naweza kusema mshindani wangu mkubwa ni wasichana wote ambao saizi wanafanya vizuri mfano Ruby, Maua, Vanessa kwa sababu wote wamekuja na tunafanya muziki ambao upo sawa, lakini mimi hainiumizi ila inanifanya nizidi kujiuliza kila siku silali, natafuta kitu cha tofauti ili niwe tofauti na Maua, nifanye nini niwe tofauti na Vanessa na nifanye nini ili niwe tofauti na Rubby” alisema Linah Sanga.

0 comments:

Post a Comment