KATIKA kila kinachotokea kwa staa kuna mengi huwa yanazungumzwa, mfano
mzuri ni baada ya msanii wa filamu Bongo, Chuchu Hans ambaye siku chache
zilizopita alibahatika Vicent Kigosi ‘ Ray’ ambapo Gazeti la Championi
limepata nafasi ya kuzungumza na Chuchu ambaye ni muigizaji wa fi lamu
kama alivyo baba watoto wake na hivi ndivyo anavyofunguka:
Championi: Mambo mama Jaden, vipi mtoto anaendeleaje?
Chuchu: Sote ni wazima wa afya.
Championi: Ni kitu gani kilichosababisha ukafi cha ujauzito, inasemekana ulikuwa unahofi a kulogwa, ni kweli?
Chuchu: Siyo kweli, sikuona kama kuna haja ya kutangaza hicho kitu, ni
mambo yangu binafsi hata kama mimi ni staa kuna vitu havihitaji
matangazo.
Championi: Ulipanga na Ray mpate mtoto kipindi hiki au ilitokea tu?
Chuchu: (Anacheka), Usawa huu hamna mimba ya bahati mbaya ni kitu ambacho tulikusudia.
Chuchu: Je, ulipendelea kumzalia Ray mtoto wa kiume kama ilivyotokea?
Chuchu: Mimi sibagui mtoto, yeyote naona sawa, ila baba yake alipenda
sana tupate mtoto wa kiume na Mungu kasikia dua yake, ndiyo maana
amefurahi kupita maelezo.
Championi: Baada ya kujifungua, Blandina Chagula ‘Johari’ ambaye ni
mkurugenzi mwenziye na Ray pale RJ Company, je ameshakuja kumuona mtoto,
japo kipindi cha nyuma mlikuwa kwenye mgogoro kwa kuwa inasemekana
aliwahi kuwa kwenye uhusiano na Ray ukampindua?
Chuchu: Siwezi kumuongelea Johari kwenye hilo kama kaja kumuona Jaden au
la, sababu siyo sehemu ya familia yangu, tuongee mengine, sioni haja ya
kumzungumzia.
Championi: Kuna mengi yalisemwa wakati mnaanzisha uhusiano wenu na Ray,
hadi kipindi cha ujauzito wako kulikuwa na tetesi za hapa na pale kuwa
mimba hiyo siyo ya Ray, uliamini pamoja na yote hayo mngefi ka hapa
mlipo leo?
Chuchu: Niliamini tungedumu na tangu tunaanza tulikuwa na malengo mengi,
likiwemo hili la kupata mtoto na kufunga ndoa, vitu vingine watu huwa
wanazusha hatukuwa na mgogoro wowote.
Championi: Hizi taarifa za kufunga pingu za maisha na Ray zina ukweli
upi na kwa nini mlifunga ndoa kimyakimya na hiyo ndoa ilifungwa lini na
wapi?
Chuchu: Ni ukweli mtupu kwamba sisi ni wanandoa, tulifunga ndoa ya siri
sababu huwa hatupendi kuanika mambo yetu hadi tuamue, muda ukifi ka kila
kitu kitakuwa wazi maana bado hatujafanya sherehe.
Championi: Mambo ya malezi yanakuathiri vipi kwenye kazi zako na je, utapumzika kwa muda gani kuigiza?
Chuchu: Hayaniathiri chochote, likitokea dili lolote mtoto akishatoka 40
nitamuachia baba yake amlee, si unajua siku hizi mambo kusaidiana.
Championi: Nini malengo yako kwenye sanaa kwa mwaka huu, baada ya mwaka
jana kutwaa tuzo ya msanii bora wa kike iliyoandalia na kituo cha EATV?
Chuchu: Malengo yangu ni makubwa mno, mashabiki watarajie kuniona kwenye
kiwango cha juu zaidi, sababu familia imeongezeka lazima nichape kazi
ipasavyo.
Championi: Unapenda mtoto wako akue kwenye mazingira yapi, awe msanii kama wewe ama?
Chuchu: Siwezi kumpangia, kikubwa naomba Mungu awe ni mtoto mwema kwa sisi wazazi wake na kwenye jamii pia.
Championi: Kwa upande wa soka unashabikia timu gani na nini kilikushawishi?
Chuchu: Naipenda sana Yanga kwa kuwa mume wangu ni shabiki mkubwa wa timu hiyo, ikifungwa amani yote huwa inatoweka nyumbani.
0 comments:
Post a Comment